Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM washirikiana na nchi za Afrika Magharibi kuinua teknolojia ya mawasiliano vyuo vikuu:

UM washirikiana na nchi za Afrika Magharibi kuinua teknolojia ya mawasiliano vyuo vikuu:

Shirika la Umoja wa Mataifa lililo na jukumu la kuchagiza elimu na muungano wa fedha wa nchi za Afrika ya Magharibi wametia saini mkataba wa kuzindua mradi wa dola milioni 12 ili kuinua uwezo wa mawasiliano na teknolojia ICT kwenye vyuo vikuu kwa kuanzisa mtandao wa mkataba wa mawasiliano wa kanda.

Irina Bokova, mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni (UNESCO), na Soumaïla Cissé, Rais wa tume ya muungano wa uchumi na fedha ya Afrika ya Magharibi (UEMOA), ambayo inatoa fedha wametia saini makubaliano mjini Paris.

Mradi huo ni sehemu ya mipango ya ushirikiano iliyoanzishwa mwaka 2006 na pande hizo mbili kwa lengo la kuanzisha matumizi ya ICT ili kusaidia mabadiliko yanayoendelea katika elimu ya juu katika nchi wanachama wa, UEMOA ambao ni pamoja na Benin, Burkina Faso, Ivory Coast, Guinea-Bissau, Niger, Mali, Senegal na Togo.

"Bi Bokova amesema elimu ya juu ni muhimu katika kuchagiza maendeleo na kuongeza kuwa kufadhili mradi huu kunaonyesha nia ya mashirika hayo kufanyia mabadiliko na kuboresha elimu ya juu kwa kuanzisha vituo vya kitaalamu.