Mwakilishi wa UM ameahidi kuendelea kuisaidia Somalia :
Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia mwishoni mwa wiki amesema jumuiya ya Kimataifa itaendelea kuisaidia serikali ya mpito ya nchi hiyo licha ya mgawanyiko uliosababishwa na kuongeza muda wa bunge na serikali kwa miaka mingine mitatu.
Mwakilishi huyo Balozi Augustine Mahiga ambaye alikuwa katikia ziara fupi nchini Somalia kuzungumza na maafisa wa serikali kuhusu uamuzi wa hivi karibuni uliofanywa na bunge la Somalia kuongeza muda wake ambalo awali ilikuwa umalizike mwezi August mwaka huu lakini sasa utamalizika miaka mitatu ijayo. Mahiga amesema amezungumza na Rais, waziri mkuu na spika wa bunge jinsi gani ya waendelee mbele kuhusu mchakato wa kumaliza serikali ya mpito. Ameongeza kuwa habari njema ni kwamba wanapata mawazo ya pamoja baina ya jumuiya ya kimataifa na viongozi wa kikanda
Kwa upande wake Rais Sheikh Sharif Sheikh Ahmed zmesema ameheshimu uamuzi wa bunge kuongeza muda wake. Ingawa serikali ya mpito imekuwa na mtazamo wa kati kuhusu kuongezwa muda waserikali hiyo, jumuiya ya kimataifa inataka muda huo umalizike kama unavyosema mkataba.
Kwa miaka sita iliyopita serikali ya Somali imeshindwa kutekeleza yake kma inavyotakiwa mkataba ikiwemo kuunda mswada wa katiba, kufanya sensa ya kitaifa na kufanya uchaguzi huru na wa haki baada ya juhudi za maridhiano ya kitaifa.