Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM yaandaa mkutano kujadilia namna ya utoaji fursa sawa kwa watuhumiwa wa ugaidi

UM yaandaa mkutano kujadilia namna ya utoaji fursa sawa kwa watuhumiwa wa ugaidi

Maafisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa, wawakilishi kadhaa wa serikali,

mahakimu pamoja na wataalamu wa haki za binadamu wanatazamiwa kukutana huko

Bangkok kujadilia namna ya uendeshwaji wa kesi katika mazingira ya haki kwa

watu wanatuhumiwa kuhusika na vitendo vya ugaidi

Kadhalika nchi hizo zimekuwa zikiweka mbinyo mkali kwa watuhumiwa hao kiasi hata kuwanyima fursa sawa kwenye vyombo vya sheria. Mkutano huo wa siku mbili ambao umeandaliwa na Umoja wa Mataifa unatazamiwa kutoa mwongozo utakosaidia kuondoa hali hiyo