Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matunda yanayolimwa kwenye milima ya Golan kusafirishwa hadi Syria

Matunda yanayolimwa kwenye milima ya Golan kusafirishwa hadi Syria

Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu ICRC imeanza kusafirisha tani 12,000 ya

matunda aina ya apple kutoka kwenye eneo lilitwaliwa la Golan na kupelekwa

nchini Syria.

Msafara kwa kwanza wa malori unatazamiwa kuanza February 15.

Matunda hayo yatasafirishwa kutoka kwa wakulima wenye asili ya Syria ambao wanaendesha shughuli zao za kilimo kwenye milima ya Golan.

Shirika hili la ICRC limekuwa likiendesha shughuli za usamaria mwema katika eneo hilo kuanzia mwaka 1967 na baadaye likapata hifadhi ya kudumu mwaka 1988.