Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yajitahidi kuwasaidia wakimbizi Watunisia waliokwama kisiwa cha Lampedusa

IOM yajitahidi kuwasaidia wakimbizi Watunisia waliokwama kisiwa cha Lampedusa

Mashirika ya kutoa misaada yanapigana kufa na kupona ili kutoa msaada wa dharura

kwa wakimbizi zaidi ya 2,000 waliokwama kwenye kisiwa cha Lampedusa, baada ya

kukosa usafiri kuwapeleka nchini Italy ambako wanatazamiwa kupewa hifadhi.

Eneo hilo linauwezo wa kuchukua watu 800 kwa wakati mmoja lakini kutokana na kundi kubwa la wakimbizi kuendelea kumiminika kwenye kisiwa hicho, kilichoko pembezoni mwa nchi ya Italy kumefanya mkusanyiko kuwa mkubwa.

Wakimbizi hao walianza kuwasili kwenye eneo hilo tangu jumatano iliyopita, na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi IOM limeonyesha wasiwasi wake kutokana na msongamano huo mkubwa wa watu.

IOM imesema kuwa wakimbizi hao hutoa kiasi kikubwa cha fedha kwa makundi ya watu wanaofanya biashara haramu ya kusafirisha binadamu jambo ambalo linahatarisha safari za watu wanaotoka Tunisia kwenda kwenye kituo hicho. Jemini Pandya ni msemaji wa IOM:

(SAUTI YA JEMINI PANDYA)