Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakazi wa mji wa Abyei waomba hifadhi UM

Wakazi wa mji wa Abyei waomba hifadhi UM

Mamia ya wananchi kutoka mji wa Abyei nchini Sudan wamekimbilia kwenye eneo

yaliyopo majengo ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuomba hifadhi kufuatia

kulipuka kwa machafuko mwishoni mwa wiki ambayo yamesababisha kuuwawa kwa watu

watatu.

Zaidi ya watu 300 wengi wao wakiwa wanaume wapo kwenye majengo hayo ya Umoja wa Mataifa tangu mwishoni mwa wiki kufuatia kuzuka kwa mapigano hayo yaliyohusisha 

vikosi vya serikali na kundi la wahalifu vijana.

Duru kutoka kwenye eneo hilo zinasema kuwa wananchi hao wanahofia kutumbukia kwenye ghasia hizo na wamelazimika kuomba hifadhi kwenye majengo hayo.