Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Leo ni siku ya kimataifa ya kupinga matumizi ya watoto jeshini

Leo ni siku ya kimataifa ya kupinga matumizi ya watoto jeshini

Dunia leo inaadhimisha siku ya kimataifa ya kupinga matumisi ya watoto jeshini, jambo ambalo ni uhalifu wa kivita.

Ofisi ya mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya watoto na migogori ya silaha imesema kuwapa mafunzo na kuwatumia watoto jeshini imekuwa ni chaguo la makundi mengi yenye silaha yanayoshirikia vitani.

Na imeongeza kuwa kikubwa cha kusikitisha ni njia wanayoitumia kuwapa mafunzo na kukaa nao ili kuwatumia vitani kama askari. Nchini Sierra Leone, kwa mfano mchanganyiko wa mihadarati kama , cocaine na unga wa risasi ulikuwa unagawiwa kwa watoto kutumia ili kuwaondoa woga na kuwapa ujasiri vitani.

Mkataba wa Roma ambao ndio nguzo ya kuanzishwa kwa mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC), umehalalisha matumizi ya watoto wenye umri wa chini ya miaka 15 vitani au kuwashirikisha katika machafuko yoyote kuwa ni kosa na ni uhalifu wa kivita.