Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ili kushinda vita dhidi ya malaria lazima ruzuku na kodi zitolewe kwenye dawa na vyandarua

Ili kushinda vita dhidi ya malaria lazima ruzuku na kodi zitolewe kwenye dawa na vyandarua

Wiki hii mkutano maalumu wa kutathimini hali ya kupambana na malaria duniani umefanyika na kutoa wito wa kuondoa kodi katika madawa ya malaria, vyandarua vya mbu na bidhaa zingine za kuokoa maisha zinazohusiana na kukabili malaria.

Mkutano huo umefanyika mjini Geneva na uliandaliwa na mpango wa kupambana na malaria Roll back malaria, mradi wa kuelimisha kuhusu viwango na kiodi katika madawa M-TAP na wadau wengine wa walio msitari wa mbele katika vita vya kudhibiti ugonjwa huo.

Mkurugenzi wa M-TAP Dr Halima Mwenesi ambaye ofisi yake iko mjini Washington Marekani anasema ili kushinda vita dhidi ya malaria na kutokomeza kabisa ugonjwa huo ifikapo 2015 ni lazima juhudi kubwa zifanyike kuondoa ruzuku na kodi na kuharakisha usafirishaji wa madawa na bidhaa zingine za kukabiliana na ugonjwa huo.

Akiwa kwenye mkutano huo mjini Geneva amezungumza na mwandishi wetu Patrick Maigua na kwanza anaeleza lengo kubwa la mradi huo.

(MAHOJIANO NA DR HALIMA MWENESI)