Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Japan yaahidi dola milioni 37.9 za msaada kwa IOM

Japan yaahidi dola milioni 37.9 za msaada kwa IOM

Serikali ya Japan imehaidi kutoa kiasi cha dola za kimarekani milioni 37.9 kwa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na uhamiaji IOM, ili kufanikisha shughuli za shirika hilo ndani ya mwaka huu 2011 pekee.

Kiasi hicho cha fedha kinatazamiwa kufanikisha kazi za shirika hilo katika nchi za Afghanistan, Kenya, Kyrgyzstan, Pakistan, Rwanda, Somalia, Sudan, Tajikistan na Tanzania.

Japan pia imehaidi kuendelea kutoa msaada wa kitaalamu ili kuzisaidia serikali mbalimbali kujijengea uwezo wa kukabiliana na tatizo mtambuka la uhamiaji wa watu. Hata hivyo kiasi kikubwa cha fedha hizo zitapelekwa nchini Pakistan ili kuwasaidia watu 450,000 waliokumbwa na mafuriko.