Hatua zahitajika kupunguza athari za pombe:WHO
Ripoti mpya ya shirika la afya duniani WHO inasema kuwa utekelezaji zaidi wa sera unahitajika ili kusaidia maisha na kupunguza athari zinazotokana na matumizi mabaya ya pombe.
Ripoti hiyo inasema kuwa matumizi mabaya ya pombe kupita kiasi unasababisha vifo vya watu milioni 2.5 kila mwaka na kusababisha magonjwa na majeraha kwa watu wemgi zaidi huku ukiwaathiri vijana na wanywaji wa pombe kwenye nchi zinazoendelea.
Matumizi mabaya ya pombe yanatajwa kuwa matumizi ya pombe kupita kiasi hadi kiwango ambapo inadhuru afya. Dr shekhar Saxena wa WHO anasema ingawa pombe inahusishwa na masula mbali mbali ya kijamii kama ugomvi ,kutowalea watoto ipasavyo na kukosa kuhudhuria kazini haipewi uzito mkubwa na serikali nyingi
(SAUTI YA SHEKHAR SAXENA)