Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vyandarua vya mbu vinasaidia kukabili malaria

Vyandarua vya mbu vinasaidia kukabili malaria

Muungano unaohusika na kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa Malaria unakutana mjini Geneva kujadili jinsi unavyoweza kupeleka kwenye knchi zingine mbinu inayotumiwa nchini Nigeria ya kugawa kwa kila mtu viandarua vya kuzuia mbu vilivyo na dawa ya kuua mbu.

Watu wote milioni 153 nchini Nigeria wanakadiriwa kuwa kwenye hatari ya kuambukizwa ugonjwa wa malaria ambapo ugonjwa huo huua mtoto mmoja kati ya watatu wanaoaga dunia wakiwa wachanga.

Inakadiriwa kuwa asilimia 50 ya Nigeria watapata maambukizi ya malaria mara moja kila mwaka huku watoto walio chini ya miaka mitano watakuwa na maambukizi mara mbili hadi nne ya ugonjwa wa malaria kila mwaka. George Njogopa anaripoti

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)