Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban kuzuru Ecuador na Peru mwishoni mwa wiki

Ban kuzuru Ecuador na Peru mwishoni mwa wiki

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon anatazamiwa kuelekea Ecuador na Peru ambako atafanya mazungumzo na viongozi wa eneo hilo.

Ziara ya Bwana Ban ambayo inaanza mwishoni mwa wiki, itaanzia nchini Ecuador. Akiwa katika nchi hiyo atakuwa na mazungumzo na mwenyeji wake rais Rafael Correa na baadaye kuzungumza na maafisa wengine wa serikali.

Baada ya hapo ataelekea katika kituo chake cha pili Peru ambako atakutana na rais Alan García.

Hii itakuwa ziara yake ya kwanza kwa Bwana Ban kufanya katika mataifa hayo mawili ya Latin Amerika