Skip to main content

Juhudi zimepigwa kuziunganisha familia zilizotenganishwa Sahara Magharibi:UM

Juhudi zimepigwa kuziunganisha familia zilizotenganishwa Sahara Magharibi:UM

Kamishina mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR Antonio Guterres na mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu Sahara Magharibi Christopher Ross wamekamilisha mkutano na serikali ya Morocco Polisario Front na nchi jirani za Algeria na Mauritania.

Mkutano huo umehitimishwa kwa habari njema kwa wote kukubaliana baadhi ya hatua za kuchukua ili kuongeza idadi ya familia za Shrawi kuonana mara kwa mara baada ya miaka 35 ya kutenganishwa.

Guterres amesema kwa zaidi ya miongo mitatu kina baba wametenganishwa na watoto wao na wake kutengwa na waume zao. Na makubaliano katika mkutano wetu yatasaidia familia nyingi kuonana tena.

Naye mkuu wa mpango wa Umoja wa Mataifa Sahara Magharibi MINURSO Hany Abdel Azizi amerejea kusisitiza nia ya Umoja wa mataifa kuendelea kutoa msaada kwa watu wa Sahara Magharibi