Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM kutathmini madeni ya nje na haki za binadamu visiwa vya Solomon:

UM kutathmini madeni ya nje na haki za binadamu visiwa vya Solomon:

Mtaalamu binafsi wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu athari za madeni ya nje katika utekelezaji wa haki za binadamu Cephas Lumina atazuru visiwa vya Solomon kuanzia Jumatatu Ijayo Februari 14 hadi 18 kutathimini athari za mzigo wa madeni ya nje kwa nchi hiyo.

Lumina ataangalia uhusiano uliopo wa madeni hayo katika kutekeleza haki za binadamu na kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia. Hii ni mara ya kwanza kabisa tathimini kama hiyo kufanyika na mtaalamu wa baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kwa kisiwa hicho. Jason Nyakundi anaarifu.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)