Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lazima tuungane kuhakikisha holocaust haitokei tena:BAN

Lazima tuungane kuhakikisha holocaust haitokei tena:BAN

MUSIC HOLOCAUST CEREMONY)

Hivyo ndivyo ilivyokuwa katika hafla maalumu ya kuwakumbunga wahanga wa mauaji ya Holocaust iliyofanyika leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa New York ikiwa na kauli mbiu "Wanawake na Holocaust, ujasiri na upendo"

Hafla hiyo imehudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo manusura,familia za baadhi ya manusura, Rais wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa Joseph Deis na naibu waziri mkuu wa Israel Ehud Barak.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema tusimame pamoja na kuahidi asilani holocaust haitotokea tena, tuwe wazi kwa wanaosema Holocaust haikutokea na kupata funzo kuhusu ubinadamu. Amesema kwa kuelimisha kizazi kipya kuhusu mauaji hayo itasaidia katika kuthamini utu wa mtu. Pia amewapongeza na kuwakumbuka wanawake waliojitolea maisha yao wakati huo ili kuokoa ya wengine.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Kila mwaka siku rasmi ya kumbukumbu hii kimataifa hufanyika Januari 27.