Wataalamu vijana kusaidia kuzipa pengo la upungufu wa maarifa

9 Februari 2011

Kundi la wataalamu wa mawasiliano ya kopyuta limeunganisha nguvu ili kuzisaidia nchi zinazoendelea ambazo zinakabiliw a na changamoto ya kufikia malengo ya maendeleo mellenia kutokana na kuendelea kubaki nyuma kwenye maarifa ya kisayansi.

Kundi hilo la wataalamu ambalo linajumuisha taasisi mbalimbali za kimataifa pamoja na zile zinazofanya kazi na Umoja wa Mataifa, limeweka shabaya ya utoaji msaada wa maarifa kwa njia ya mitandao ili nchi zilizo maskini ziweza kufukia pengo la kukosa maarifa ya kutosha.

Wataalamu hao wanakusudia kuchapisha na kusambaza taarifa zenye maarifa ya kisayansi na ya kiutafiti kwenye majarida mbalimbali ambayo yatafikiwa na nchi nyingi zinazojingongoja kimaendeleo.

Mowajapo ya kampuni iliyounganisha nguvu hizo kampuni ya Microsoft imeshatoa wito kwa wanafunzi zaidi ya 325,000 ambao wamejiandikisha kwenye mitandao duniani kote kuzalisha mfumo maalumu wa kushusha taarifa toka kwenye internet ili iwe rahisi kwa watumiaji wa viwango vya chini kukusanya taarifa na kuzitumia.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter