Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko ya amani ndiyo yanayohitajika Misri:Ban

Mabadiliko ya amani ndiyo yanayohitajika Misri:Ban

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amesema kuwa ni lazima Misri iyasikilize matakwa ya watu wake.

Akiongea na waandishi wa habari baada ya baada ya kulihutubia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa Ban amesema kuwa anaamini matamshi yake ya hapo awali hayatazua utatanishi alipokuwa akitoa wito kwa serikali ya Misri kufanya mashaurino na wananchi wake ambao wamekuwa wakiandamana wakitaka kuwepo mabadiliko kwa muda wa majuma mawili yaliyopita.

Ban anasema kuwa wananchi wa Misri wamekatishwa tamaa na sasa wanataka kuwe na mabadiliko na hivyo ni lazima viongozi wa Misri au wa nchi yoyote ile duniani kusikiliza kwa makini matakwa ya watu wao.

Awali Ban alikutana na balozi wa Misri kwenye Umoja wa Mataifa kujadili hali nchini mwake lakini hata hivyo balozi huyo anasema kuwa hakuna mawasiliano kamili kuhusu masuala fulani ya kile ambacho kimekuwa kikiendelea nchini Misri.