Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kodi ziondolewe katika madawa na vyandarua vya mbu:M-TAP

Kodi ziondolewe katika madawa na vyandarua vya mbu:M-TAP

Mkutano maalumu wa kutathimini hali ya kupambana na malaria duniani umetoa wito wa kuondoa kodi katika madawa ya malaria, vyandarua vya mbu na bidhaa zingine za kuokoa maisha zinazohusiana na kukabili malaria.

Mkutano huo unaofanyika mjini Geneva na umeandaliwa na mpango wa kupambana na malaria Roll back malaria, mradi wa kuelimisha kuhusu viwango na kiodi katika madawa M-TAP na wadau wengine wa kudhibiti ugonjwa huo. Mkurugenzi wa M-TAP Dr Halima anasema ili kushinda vita dhidi ya malaria ya kutokomeza kabisa ugonjwa huo ifikapo 2015 ni lazima juhudi kubwa zifanyike kuondoa ruzuku na kodi na kuharakisha usafirishaji wa madawa na bidhaa zingine za kukabiliana na ugonjwa huo.

(SAUTI YA DR HALIMA MWENESI)