Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama litume ujumbe Mashariki ya Kati:Urusi

Baraza la usalama litume ujumbe Mashariki ya Kati:Urusi

Balozi wa Urusi kwenye Umoja wa Mataifa Vitaly Churkin amependekeza kwamba baraza la usalama la Umoja wa Mataifa litume ujumbe maalumu kuzuru Mashariki ya Kati.

Bwana Churkin amesema pendekezo lake ni kutokana na ukweli kwamba hakujakuwa na ujumbe wowote wa baraza la usalama Mashariki ya Kati tangu mwaka 1979 jambo ambalo analiona si sahihi.

Ameongeza kuwa hiyo sio sababu pekee ya ya kutaja ujumbe wa baraza la usalama upelekwe Mashariki ya Kati, kikubwa ni hofu walioyo nayo kuhusu hali nzima ya mashariki ya kati na anadhani ujumbe huo utakuwa msaada mkubwa.

(SAUTI YA CHURKIN)

Amesema ujumbe utakaopelekwa mbali ya kuzuru Israel na himaya ya Palestina pia itakuwa muhimu kutembelea Misri ambako kunakabiliwa na machafuko ya kisiasa hivi sasa, Lebanon na Syria.