Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi zinazoendelea zimetakiwa kuwekeza katika kuzuia na kupunguza majanga:UM

Nchi zinazoendelea zimetakiwa kuwekeza katika kuzuia na kupunguza majanga:UM

Nchi zinazoendelea zimetakiwa kuwa na ari ya kisiasa ya kuwekeza katika mipango ya kupunguza au kuzuia majanga.

Umuhimu wa kujiandaa kwa ajili ya majanga ili kuokoa maisha ya mamilioni ya watu na fedha umejadiliwa kwenye baraza kuu la Umoja wa Mataifa kwa mara ya kwanza. Mwaka 2010 majanga ya asili zaidi ya 373 yalitokea duniani kote na kukatili maisha ya karibu watu 300,000 na kuathiri wengine zaidi ya milioni 200.

Mwakilishi maalumu wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataika katika upunguzaji wa hatari ya majanga Bi Margareta Wahlstrom amesema kujiandaa kwa majanga ni hatua muhimu katika mchakato wa maendeleo.

(SAUTI YA MARGARETA WAHLSTROM)