Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua kubwa inahitajika kujumuisha wanawake katika ulinzi:UM

Hatua kubwa inahitajika kujumuisha wanawake katika ulinzi:UM

Miaka kumi baada ya Umoja wa Mataifa Tkutoa wito wa kuhusishwa zaidi kwa wanawake katika masuala ya amani, mpango wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa una takwimu mchanganyiko kuhusu suala hilo na unataka juhudi ziongezwe kufikia lengo.

Hayo yamo kwenye utafiti uliozinduliwa leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa. Utafiti huo ni wito wa kuchukuliwa hatua kwa viongozi wa ngazi za juu wa masuala ya kulinda amani kuchapusha utekelezaji wa azimio namba 1325.

Hayo ameyasema mkuu wa Umoja wa Mataifa wa operesheni za kulunda amani, Alain Le Roy akikumbusha azimio hilo la baraza la usalama lililopitishwa Oktoba 2000 likiwa na lengo la kutokomeza ukatili wa kimapenzi dhidi ya wanawake na wasichana katika maeneo ya vita na kuchagiza ushiriki wa wanawake katika masuala ya kulinda amani.

Utafiti huo umefanywa na idara ya mipango ya kulinda amani DPKO na idara ya msaada kwa walio nje DFS na umetoa wito kwa mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinnda amani kufanya kazi na wanawake mashinani, uongozi wa serikali na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuongeza idadi ya ushiriki wa wanawake katika mjadiliano, taasisi za usalama wa taifa na utawala katika maeneo yaliyotoka kwenye hali ya vita.

Ulinzi wa amani umekuwa na jukumu kubwa katika hatua zilizopigwa katika ushiriki wa wanawake kwenye masuala ya siasa kama wapiga kur, wagombea na maafisa waliochaguliwacandidates , mfano mzuri ukijitokeza katika nchi ambazo mfumo wa kugawana viti unatekelezwa kama Timor-Leste na Burundi.