Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama laainisha umuhimu wa ushirikiano baina ya UM, EU na jumuiya zingine

Baraza la usalama laainisha umuhimu wa ushirikiano baina ya UM, EU na jumuiya zingine

Muungano wa Ulaya (EU) leo umerejea kusistiza nia yake ya kuendeleza mshjikamano kupitia Umoja wa Mataifa ulio imara.

Jumuiya za kikanda zinawajibu mkubwa katika utawala na majukumu ya kimataifa kwanza kuhakikisha usalama, maendeleo na haki za binadamu katika maeneo yao, na pili kuunga mkono juhudi za Umoja wa Mataifa kupigia chepuo malengo haya duniani kote , amesema mwakilishi wa sera za mambo ya nje na usalama wa nchi 27 za muungano wa Ulaya Catherine Ashton, kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Akihutubia baraza hilo la wajumbe 15 kama sehemu ya tathimini ya ushirikiano baina ya Umoja wa Mataifa na jumuiya za kikanda Bi Ashton ameainisha masuala mengi yanayochukuliwa hatua kwa ushirikiano baina ya Muungano wa Ulaya na Umoja wa Mataifa akitolea mfano ushiriki wa Quartet kati ya Muungano wa Ulaya, UM, Urusi, na Marekani unaotafuta suluhu ya kuwa na mataifa mawili katika mzozo wa Mashariki ya Kati baina ya Israel na Palestina.

Akizungumzia maandamano Afroika Kaskazini na Mashariki ya Kati watu wakitaka ushiriki wa kisiasa, uhuru, haki na maendeleo Bi Ashton ametoa ujumbe ambao umerejewa mara kadhaa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kwamba masuala hayo ni muhimu kutekelezwa ili kuleta amani na utulivu.