Hatua za kuleta utulivu DRC zaanza kuonekana:UM

8 Februari 2011

Wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo anafanya jitihada za kuleta utulivu katika taifa hilo hata ingawa jitihada hizo kwa sasa zinakabiliwa na ukosefu wa fedha na vifaa vya kijeshi.

Mwakilishi maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini DRC Roger Meece anasema kuwa jitihada zaidi zinahitajika ili kukabiliana na vitendo vya ubakaji vinavyotumiwa kama silaha na waasi pamoja na wanajeshi wa serikali na pia kuwabadili waasi wa zamani.

Meece amesema kuwa kuwahakikishia usalama raia kutoka kwa makundi yaliyojihama imesalia kuwa ajenda yao kuu hususan baada ya tukio la mwezi uliopita ambapo watu 80 walibakwa na waasi wa kunndi la FDLR wanaotumia ubakaji kama silaha dhidi ya raia.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter