Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mafuriko yaliyozuka tena Sri Lanka yamesababisha athari kubwa:OCHA

Mafuriko yaliyozuka tena Sri Lanka yamesababisha athari kubwa:OCHA

Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA linasema mafuriko ya awamu ya pili nchini Sri Lanka yamesababisha athari kubwa kuliko ya kwanza.

Mafuriko hayo yameathiri mashamba ya mpungua na mazao mengine huku yakiwaacha watu milioni 1.1 bila makao na kusababisha vifo 14. Watoto wamearifiwa kuwa katika hatari zaidi kwani wengi wao hawawezi kuongelea limesema shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF.

Hivi sasa UNICEF inasambaza misaada katika wilya mbalimbali zilizoathirika. Misaada hiyo ni pamoja na vifaa vya shule 19,000 vinvyojumuisha kalamu, madaftari na penzeli, dawa ya clorine ya kusafisha maji, magodoro ya kulalia, madumu ya kuhifadhi maji na nguo. Nalo shirika la mpango wa chakula duniani WFP limesema linaongeza msaada wa chakula kwa waathirika kama anavyofafanua msemaji wa shirika hilo Emilia Casella.

(SAUTI YA EMILIA CASELLA)