Skip to main content

Waomba hifadhi 8 wamekufa wakiwa njiani kwenda Afrika Kusini:UNHCR

Waomba hifadhi 8 wamekufa wakiwa njiani kwenda Afrika Kusini:UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema waomba hifadhi wanane wamefariki dunia baada ya kukosa hewa ndani ya lori wakiwa njiani nchini Msumbiji.

Waomba hifadhi hao ambao ni raia wa Ethiopia walikuwa wakisafiri kwenye lori lililofunikwa tarehe pili ya mwezi huu. Polisi wanasema marehemu hao walikuwa miongoni mwa kundi la vijana 26 wa Kiethiopia waliokuwa wakijaribu kwenda Afrika ya Kusini kutoka kambi ya wakimbizi ya Maratane Kaskazini mwa Msumbiji. Jason Nyakundi na ripoti Kamili

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)