Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ingawa kumejitokeza athari lakini chanjo ya mafua bado muhimu:WHO

Ingawa kumejitokeza athari lakini chanjo ya mafua bado muhimu:WHO

Shirika la afya duniani WHO limesema chanjo ya mafua iliyosababisha athari za kusinzia au Narcolepsy miongoni mwa watoto na vijana haitoondolewa kwenye soko.

Nchi 12 zimearifu ongezeko la visa vya kusinzia kwa watoto na vijana wa kati ya umri wa miaka 4 hadi 19baada ya kupewa chanjo dhidi ya virusi vya H1N1 iitwayo Pandemrix.

Idadi kubwa ya walioapata ugonjwa wa Narcolepsy ambao huwafanya watu kusinzia ghafla na bila kutegemewa imeripotiwa Finland, Sweeden na Iceland. Kwa mujibu wa msemaji wa WHO Alison Brunier uhusiano kati ya chanjo hiyo na ugonjwa wa kusinzia bado unachunguzwa lakini kwa sasa Pandemrix itasalia kuwa sehemu ya njanzo inayopendekezwa na WHO kwa msimu wa 2010/2011.

(SAUTI YA ALISON BRUNIER)

Chanjo ya Pandemrix inatengenezwa na kampuni ya madawa ya GlaxoSmithKline. WHO inasema hivi karibuni ilitoa msaada wa chanjo dizi milioni 36 kwa nchi 18 duniani kote.