Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali ya Sudana na UNAMID kufanya mkutano wa kimataifa wa maji Darfur

Serikali ya Sudana na UNAMID kufanya mkutano wa kimataifa wa maji Darfur

Jimbo la Darfur Sudan linakabiliwa na uhaba mkubwa wa maji suala ambalo linaonekana kuwa moja ya sababu ya machafuko ya kikabila hasa kutoka jamii za wakulima na wafugaji.

Kwa kulitambua hilo mpango wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika Darfur UNAMID umeamua kuitisha mkutano wa kimataifa kwenye jimbo hilo kwa lengo la kuhamasisha haja ya kulisaidia jimbo la Darfur kupata maji, na pili ni kuchangisha fedha zitakazotumia kufadhili miradi zaidi ya maji kwenye jimbo hilo.

Serikali ya Sudan kwa ushirikiano na UNAMID wako msitari wa mbele kufanikisha mkutano huo. Mwandishi wetu wa Darfur Stella Vozo amezungumza na Emmanual Mollel ambaye ni mkuu wa kitengo cha cha utunzi wa mazingira katika kikosi cha UNAMID anaeanza kwa kufafanua lengo kuu la mkutano huo.

(MAHOJIANO NA MOLLEL)