Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akaribisha uchaguzi wa waziri mkuu mpya Nepal

Ban akaribisha uchaguzi wa waziri mkuu mpya Nepal

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha kuchaguliwa kwa Jhalanath Khanal kuwa Waziri Mkuu wa Nepal, hatua ambayo inamaliza miezi kadhaa ya hali tete iliyoiandama nchi hiyo.

Hatua hiyo pia inatoa njia ya kuundwa kwa serikali mpya ambayo itasukuma mbele ustawi wa nchi hiyo iliyoko kusin mwa Asia.

Ban amehaidi kuwa Umoja wa Mataifa uko nyuma ya Nepal ili kuisaidia nchi hiyo iliyoko kwenye mchakato wa uundwaji wa katiba mpya. Katiba hiyo inatazamiwa iwe imekamilika mwishoni mwa May mwaka huu.