Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yawaandikisha watu 25,000 waliohama makwao nchini Pakistan

UNHCR yawaandikisha watu 25,000 waliohama makwao nchini Pakistan

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa limewaandikisha watu 25,000 waliolazimika kuhama makwao kufuatia oparesheni mpya zinazoendeshwa na jeshi ndidi ya wanamgambo kaskazini magharibi mwa Pakistan.

UNHCR inasema kuwa iwapo mapigano hayo yataongezeka huenda karibu watu 90,000 wakakimbia makwao ifikapo mwishoni mwa mwezi huu. Kwa sasa UNHCR imebuni makambi mawili ambayo watachukua hifadhi watu ambao wamekuwa wakikimbia maeneo ya Sagi na Dawazei tangu kuanza kuchacha kwa oparesheni za kijeshi tarehe 27 mwezi Januari. Wengi wa wanaowasili kwenye kambi hawana chochote bali nguo tu na kwa sasa kinachohitajika ni mavazi ya msimu wa barini pamoja na makao