Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yaitaja tohara ya wasichana kama dhuluma na isiyo na manufaa

WHO yaitaja tohara ya wasichana kama dhuluma na isiyo na manufaa

Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa tohara ya wasichana ni ukiukaji wa haki za binadamu za wasichana na wanawake.

Inakadiriwa kuwa wasichana milioni 140 pamoja na akina mama wamepashwa tohara huku wasichana milioni wakiwa kwenye hatari ya kupashwa tohara kila mwaka. WHO inasema kuwa hata kama upashaji tohara wasichana na wanawake umepungua kwa asilimia 50 bado kuna nchi zinazoendesha vitendo hivyo zikiwemo Djibouti, Misri, Eritrea, Guinea, Sierra Leone na Somalia.

(SAUTI YA DR ELISE JOHANSSON)