Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapigano yasababisha vifo zaidi Moghadishu:UNHCR

Mapigano yasababisha vifo zaidi Moghadishu:UNHCR

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa takriban watu 15 wameuawa na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa kufuatia kuzuka kwa mapigano mapya kwenye mji mkuu wa Somali Mogadishu.

UNHCR inasema kuwa imehusunishwa na mauaji hayo ambapo imetoa wito kwa makundi yaliyojihami kwenye mji mkuu kuweka kipaumbe usalama wa raia. Adrian Edwards ni msemaji wa UNHCR mjini Geneva.

(SAUTI YA ADRIAN EDWARD)

UNHCR inakadiria kuwa watu milioni 1.5 wamelazimika kuhama makwao ndani ya nchi na wengine zaidi ya 650,000 wanaishi kama wakimbizi kwenye nchi majirani .