MONUSCO wawaokoa polisi waliotekwa DRC

3 Februari 2011

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa kwenye Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wamewaokoa polisi sita waliotekwa nyara na waasi biIa ya kulipa fidia wala kufyatuliwa kwa risasi lakini kwa njia ya kidiplomasia.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq anasema kuwa wanajeshi wa Umoja wa Mataifa katika kambi ya Ntoto kwenye mkoa wa Kivu Kusini walijulihswa kuhusu utekaji nyara huo uli0fanya na kundi la mai mai ambapo wanajeshi hao walichukua hatua za haraka na kuizungka nyumba walimokuwa.

Haq anasema kuwa hapo ndipo walimpata afisa wa polisi wa ngazi ya juu na wenzake watano ambapo wanajeshi kutoka India walitumia mazungumzo kupata polisi hao kuachiliwa.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud