Zambia kuwapa umeme watu wake kupunguza ukataji miti

Zambia kuwapa umeme watu wake kupunguza ukataji miti

Serikali ya Zambia imesema inajitahidi kwa kila njia kuwaelemisha watu wake athari za ukataji miti kwa mazingira na maisha yao.

Nchi hiyo ambayo ni moja ya nchi masikini duniani asilimia kubwa ya watu wake wanaishi vijijini na wanatumia kuni kama nishati ya kupikia, hali ambayo inaongeza tatizo la ukataji miti. Hata hivyo serikali ya Zambia inasema sasa imeshikia bango changamoto hiyo na inatumia njia mbalimbali kukabiliana nalo.

Akizungumza kwenye mkutano wa uzinduzi wa mwaka wa umuhimu wa misitu kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa New York waziri wa utalii, mazingira na malia asili wa Zambia Bi Catherine Namulanga amesema moja ya njia kubwa wanayoitumia ni kuwapatia wananchi nishati mbadala ambayo ni umeme na pia kuwaelimisha.

(SAUTI YA CATHERINE NAMULANGA)