Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maharamia 750 wanashikiliwa katika nchi 14:UNODC

Maharamia 750 wanashikiliwa katika nchi 14:UNODC

Idadi ya maharamia wa Kisomali wanaoshikiliwa katika nchi 14 duniani hivi sasa imefikia 750 kwa mujibu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya madawa na uhalifu UNODC.

Ofisi hiyo inakadiria kwamba mashambulizi dhidi ya meli yaliyofanywa na maharamia kwenye bahari ya Hindi yanagharimu dola bilioni 7 kwa mwaka huku dola milioni 200 zikilipwa kama kikombozi.

Alan Cole kutoka UNODC Afrika ya Mashariki anasema suluhisho la muda mrefu la tatizo la uharamia linategemea mabadiliko ya mfumo wa sheria na kuchagiza maendeleo.

(SAUTI YA ALAN COLE)