Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hukumu ya kunyongwa inatekelezwa sana Iran:UM

Hukumu ya kunyongwa inatekelezwa sana Iran:UM

Mkuu wa tume ya haki za bidamu ya Umoja wa Mataifa Navi Pillay anasema kuwa takriban watu 66 wamenyongwa nchini Iran kutokana na makosa kadha ya uhalifu tangu kuanza kwa mwaka huu.

Wengi wa walionyongwa walipatikana na makosa yanayohusiana na madawa ya kulevya lakini hata hivyo anasemekana kuwa wafungwa watatu wa kisiasa ni kati ya walionyongwa. Pillay anasema kuwa ameshangazwa na hatua za Iran za kutumia hukumu ya kifo baada ya wito wake wa kuitaka Iran kusitisha hukumu hiyo.

Pillay anasema kuwa kunyongwa kwa wafungwa wa kisiasa ni jambo linalohusunisha na pia hakubaliki watu kufungwa kwa kuhusika na makundi ya upinzani. Anasema kuwa Iran ni mwanachama wa makubaliono ya kimataifa ya haki za kisiasa ambayo yanatoa ruhusa ya haki ya kujieleza na kukutana akiongeza kuwa watu wengi bado wanakabiliwa na hukumu ya kifo wakiwemo wafungwa wa kisiasa.