Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban awataka Wasudan kutulia uhesabuji kura ukikamilika

Ban awataka Wasudan kutulia uhesabuji kura ukikamilika

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezitaka pande zote za Sudan ambazo zilitia saini makubaliano ya kumaliza machafuko kati eneo la Kaskazni na Kusin kujizuia na vitendo vyovyote vinavyoweza kuharibu amani, wakati huu ambapo zoezi la uhesabuji wa kura za maoni likikaribia kumalizika.

Tangu kumalizika upigaji wa kura ya maoni iliyoanza hapo January 9 -15 ambayo ni matokeo ya mkataba wa amani uliofikiwa mwaka 2005,uliomaliza miongo kadhaa ya machafuko, zoezi la uhesabuji kura limeendelea kwa majuma kadhaa na sasa linafikia ukingoni.

Hata hivyo matokeo ya awali ya kura hizi zinaonyesha kuwa wananchi wa Sudan Kusin wanaunga mkono wazo la eneo hilo kujitenga kutoka kwa himaya ya Sudan na kuwa dola yake yenyewe.

Akizungumzia mchakato huo, Ban amesema kuwa wananchi wa Sudan wamefika hapala pa kuandika historia mpya hivyo pande zote zinapaswa kujutuliza sasa na kuendelea kuheshimu makubalino hayo ya amani ambayo ndiyo yaliyozaa kura hiyo ya maoni.