Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wadau wa biashara sasa kuweza kulinganisha viwango kwenye wavuti

Wadau wa biashara sasa kuweza kulinganisha viwango kwenye wavuti

Wazalishaji, wasafirishaji na wanunuzi sasa wanaweza kulinganisha kwa hiyari bidhaa mbalimbali katika sehemu moja.

Sehemu hiyo ni wavuti ya kituo cha kimataifa cha biashara ITC ambacho kimeweka ramani ya viwango mbalimbali. Wavuti hiyo iitwayo www.standardmap.org ni ya kwanza yenye takwimu za viwango kama vya soko huria, baraza la masuala ya misitu na baraza la masuala ya viumbe vua majini. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Kipimo hicho ambacho kwa lugha nyingine kinaweza kujulikana kama ramani ya ubora, kinataratibiwa na kuendeshwa na taasisi zisizo za kiserikali pamoja na sekta binafsi na kwamba watu wanaopenda kukutumia hawabanwi na sheria na wanaweza kufanya hivyo kwa hiari yao wenyewe.

Hata hivyo kuna dhana kwamba pamoja na utumiaji wa chombo hiki ni wa hiari lakini wachunguzi wa mambo wanaona kwamba ni fursa nzuri inayoweza kukaribisha hali ya uwazi kwenye masoko ya biashara jambo ambalo pia linaweza kukaribisha kuwepo kwa mazingira endelevu ya uendeshaji biashara wenye viwango vyenye kukubalika.

Mfumo huo umeletwa kama hatua ya kuwafungua macho wafasarishaji wa eneo la Kusin ambao wamekuwa na shabaya kubwa ya kupeleka bidhaa zao kwenye masoko ya nchi zilizoendelea. Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa la bidhaa kutoka kwenye eneo hilo hivyo kuwepo kwa mfumo huo kutasaidia kujibu maswali mbalimbali yanayoibuka ikiwemo yale yanayotaka  taarifa sahii na katika mazingira ya uwazi na ukweli.