Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wa Ivory Coast kupata chanjo ya surua Liberia:UNICEF

Wakimbizi wa Ivory Coast kupata chanjo ya surua Liberia:UNICEF

Kampeni ya chanjo ya surua inayowalenga watoto wote kwenye jimbo la Nimba nchini Liberia linalohifadhi wakimbizi wa Ivory Coast zaidi ya 30,000 inaanza kesho Jumatano.

Kampeni hiyo ya wiki moja inafanyika kwa ushirikiano wa shirika la kuhudumia watoto UNICEF na shirika la afya duniani WHO.

Tanfu mwishoni mwa mwezi Januari mwaka huu watoto watano wa Liberia wenye umri wa miaka kati ya mmoja na mitano wamekufa kutokana na surua , na visa vingine viwili vimethibitishwa na WHO huku vingine zaidi ya 100 vimeripotiwa.

UNICEF inasema katika jimbo hilo watu ni wengi, kuna upungufu wa chakula, maji safi, usafi na huduma za afya. Msemaji wa UNICEF nchini Liberia ni Christopher Tidey.

(SAUTI YA CHRISTOPHER TIDEY)