Wakristo Iraq bado wanakabiliwa na vitisho:IOM

Wakristo Iraq bado wanakabiliwa na vitisho:IOM

Wakristo nchini Iraq wanaendelea kukabiliwa na vitisho vya ghasia miezi mitatu baada ya shambulio katika kanisa la Saidat al-Najat mjini Baghdad.

Katika taarifa zilizotolewa karibuni kuhusu Wakristo kuzikimbia nyumba zao mjini Baghdad shirika la kimataifa la uhakimiaji IOM linasema , maelfu ya Wakristo wanakabiliwa na matatizo makubwa, kwanza ni usalama wao licha ya ongezeko la ulinzi na vituo vya ukakuguzi barabarani na karibu na nyumba zao, lakini pili wanakabiliwa na matatizo ya kiuchumi. Jason Nyakundi anaripoti.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Kuendelea kuwepo kwa ukosefu wa usalama kumewalazimu wakiristo wengi kuhama makwao huku shirika la kimataifa la uhamiaji IOM likisema kuwa kwa sasa zaidi ya wakiristo 1300 wanatafuta hifadhi katika maeneo ya kaskazini ya Erbil, Dahuk, Sulaymaniyah na Ninewa.

Hali hii inayosababisha wakiristo kuhama makwao pia imezua kutokea msukosuko wa kiuchumi baada ya kuenezwa uvumi kuhusu ghasia zinazoendeshwa dhidi ya wakiristo kama moja ya njia ya kuwafanya wakiristo kukimbia makwao na kuuza nyumba zao kwa bei ya chini. Wengi wa waliohama wanaishi kwenye nyumba za kukodisha ambapo kodi ni ya juu zaidi.

Shirika la IOM limegundua kuwa katika maeneo mengine yaliyo na idadi kubwa ya wakiristo waliohama makwao kodi zimaongezeka kwa kati ya asilimia 200-300 tangu mwezi Novemba mwaka uliopita wakati wakisrito walipoanza kuhama makwao.