Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchunguzi wa athari za chanjo ya mafua wafanyika:WHO

Uchunguzi wa athari za chanjo ya mafua wafanyika:WHO

Idadi kubwa ya watoto na vijana nchini Finland, Iceland na Sweeden wamearifiwa kukumbwa na tatizo la kusinzia baada ya kupata njacho ya mafua kwa ajili ya msimu wa baridi.

George Hartl kutoka Who anasema athari za chanjo hiyo zimejitokeza katika nchi tatu tuu za Ulaya, lakini shirika hilo limezambaza dozi milioni 36 za chanjo ya pandemrix kwa nchi 18 duniani.

(SAUTI YA GEORGE HARTL)

Shirika la WHO limesema licha ya kujitokeza kwa athari hizo inapendekeza matumizi ya chanjo ya msimu wa baridi ya mafua kwa watoto na vijana iendelee.