Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afghanistan yaingia mkatana na UM kutoingiza watoto jeshini

Afghanistan yaingia mkatana na UM kutoingiza watoto jeshini

Umoja wa Mataifa na serikali ya Afghanistan wametia sahihi makubaliano ambapo Afghanistan ilikubali kusaiadia watoto walioathirika na mizozo na pia kuzuia kuingizwa watoto kwenye jeshi.

Akitia sahihi makubaliano hayo pamoja na mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya watoto na mizozo waziri wa masuala ya kigeni wa Afghanistan Zalmai Rassoul amesema kuwa hii ni hatua kubwa kwa siku nzuri za baadaye kwa watoto wa Afghanistan.

Mwezi Aprili mwaka uliopita idara ya polisi ya Afghanistan ilitajwa kwenye ripoti ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kama inayohusika kwa kuwaajiri watoto. Serikali pia imechukua jukumu la kuzungumza na makundi yaliyojihami ili yaweze kuwaachilia watoto wanaohudumu kwenye makundi hayo walio chini ya miaka 18.