Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNDP imesaidia katika uchaguzi wa Jumapili Niger

UNDP imesaidia katika uchaguzi wa Jumapili Niger

Shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP limeupongeza uchaguzi uliondaliwa nchini Niger ambao ni uchaguzi wa kwanza wa kumchagua rais na bunge unaomaliza kupindi cha uongozi wa kijeshi na kuilekeza nchi hiyo kwenye uongozi wa kiraia.

Mwakilishi wa UNDP nchini Niger Khardiata Lo N'Diaye anasema kuwa uchaguzi huu unaashiria kurejea kwa mfumo wa uongozi utakaoshughulikia masuala ya kimaendeleo akisema kuwa elimu kwa wanawake , utulivu na usalama wa chakula vinastahili kupewa umuhimu mkubwa.

Mwaka uliopita serikali ya Niger ikiungwa mkono na Umoja wa Mataifa iliendesha kampeni ya misaada ya kibinadamu na kukabiliana na tatizo la uhaba wa chakula lililokuwa limeyaweka hatarini maisha ya zaidi ya watu milioni saba.