Ban azungumza na viongozi wa Rwanda na Ufaransa

31 Januari 2011

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekuwa na mazungumzo na viongozi wa Ufaransa na Rwanda ambako wamejadilia masuala mbalimbali ikiwemo shabaya ya Umoja huu wa Mataifa kuendelea kushirikiana na mataifa hayo.

Ban ambaye anahudhuria kikao cha Umoja wa Afrika huko Addis Ababa, amemuhakikishia rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy kuwa Umoja wa Mataifa uko tayari kuendelea kufanyakazi kwa karibu kundi la nchi 20 zilizoendelea kiuchumi na zile zinazoanza kuibukia ili kubuni na kuendesha miradi ya kimaendeleo.

Viongozi hao wawili pia wamejadilia hali ya kisiasa nchini Côte d'Ivoire,na raia Sarkozy amekaribisha hatua iliyochukuliwa na Umoja wa Afrika ya kuunda chombo maalumu kitachofuatilia kwa karibu hali ya mizozo katika eneo la afrika magharibi. Kwa upande wa pili Ban amekutana na kufanya mazungumzo na rais wa Rwanda Paul Kagame.

Wote wameunga mkono juhudi zinazoendelea kufanywa ili kustawisha hali ya amani kwenye eneo la maziwa makuu. Pia wamejadilia haja ya kuchukuliwa hatua zaidi ili kukomesha vitendo vya unyanyasaji kijinsia kwenye maeneo yaliyokubwa na migogoro.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter