Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wimbi jipya la mabadiliko sasa linasambaa Afrika:Ban

Wimbi jipya la mabadiliko sasa linasambaa Afrika:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa wimbi jipya la mabadiliko sasa linasambaa kote barani afrika na wananchi wake wameanza kupata fursa kwenye changuzi na pia kushamiri kwa mageuzi ya kiuchumi.

Ban ambaye alikuwa akizungumza kwenye mkutano wa Umoja wa Afrika unaofanyika huko Addis Ababa Ethiopia, amesema mabadiliko ya kiuchumi ambayo sasa yanakuwa ni kiashirio kipya ndani ya bara la afrika.

Hata hivyo amewataka viongozi wa afrika kutoa kipaumbele katika maeneo matatu ambayo ameyataja kuwa ni wanawake, vijana na sekta binafsi. Kwenye hotuba yake hiyo ambayo imekugusia masuala mbalimbali, Ban amewataka viongozi hao wa afrika kusaidia Tunisia kwenye mchakato wa uundwaji wa serikali ya muda ambayo inahusisha makundi yote.