Matumizi ya samaki duniani sasa yameongezeka yasema FAO

31 Januari 2011

Mchango wa samaki katika mlo wa binadamu duniani umeongezeka sana na kufikia rekodi ya wastani wa kilo 17 kwa mtu mmoja na kuwalisha watu zaidi ya bilioni tatu wakichangia asilimia 15 ya protin ya wanyama inayoliwa na binadamu.

Takwimu hizi ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa leo ambayo inaelezea hali ya uvuzi na na shirika la chakula duniani FAo ambayo inasema ongezeko hili la mahitaji ya samaki ni kutokana na kukua kwa uzalishaji wa viumbe vya majini.
Ripoti hiyo pia inasisitiza kwamba hali ya akiba ya samaki duniani bado haijaimarika. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud