Umoja na mshikamano ndio suluhu ya matatizo yaliyo Afrika

Umoja na mshikamano ndio suluhu ya matatizo yaliyo Afrika

Umoja, mshikamano na msiamamo wa pamoja ndio suluhu ya matatizo makubwa yanayoighubika Afrika hivi sasa.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akizungumza na waandishi wa habari mjini Addis Abba nchini Ethiopia. Amesema Afrika hivi sasa inakabiliwa na changamoto kubwa kukiwa na matatizo kama mvutano wa kisiasa unaondelea Ivory Coast, suala la Sudan na Somalia ambayo amesema ni changamoto zinazohitaji ushirikiano na kuwa na msimamo wa pamoja. Akisisitiza umuhimu wa kutatua mzozo wa kisiasa Ivory Coast Ban amesema.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)