Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake Afrika wawe mbele katika uongozi: Ban

Wanawake Afrika wawe mbele katika uongozi: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewataka wanawake barani Afrika kujitokeza kutekeleza haki zao za kuketi katika meza ya majadiliano, yaani kujihusisha katika uongozi, wa kisiasa, bunge na jamii kwa ujumla.

Ban ametoa wito huo mjini Addis Ababa Ethiopia wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa kitengo cha Umoja wa Mataifa cha wanwake UN barani Afrika. Hafla hiyo imefanyika sambamba na mkutano wa ngazi za juu wa viongozi wa muungano Afrika nchini humo. Ban amezungumzia mapambazuko ya muungo wa wanawake barani Afrika.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Amesisitiza haja ya kuwawezesha wanawake barani Afrika ambao ndio wazalishaji wakubwa wa chakula,waleaji wa watoto na waendeshaji wa uchumi. Amewataka wanawake wengi kujihusisha kataika madaraka ili uwezo wa bara la Afrika uonekane.