Skip to main content

UM na Afrika lazima tuungane kuhakikisha matokeo ya uchaguzi yanaheshimiwa:Ban

UM na Afrika lazima tuungane kuhakikisha matokeo ya uchaguzi yanaheshimiwa:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo ameelezea hatua ambazo amesema zitaongoza juhudi za kutatua mzozo wa kisiasa nchini Ivory Coast, zikiwemo madai kwamba Rais Laurent Gbagbo aachie madaraka na kuruhusu kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa itakayoongozwa na Rais aliyechaguliwa Alassane Ouattara.

Kizungumza kwenye mkutano wa ngazi za juu wa muungano wa Afrika kuhusu Ivory Coast kwenye makao makuu ya muungano huo AU mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, Bwana Ban amesema kwamba kuyarejea tena matokeo ya urais itakuwa ni kutotenda haki na kuonyesha mfano mbaya .

Ameongeza kuwa wajibu wetu wa kwanza ni kwa watu wa Ivory Coast, tuna jukumu la kuwa na msimamo imara na wa pampja na kuwaonyesha watu wa Afrika kwamba jukumu letu kwa misingi tuliyoweka ni ya kweli,msimamo wetu dhidi ya Bwana Gbagbo anayetaka kung'ang'ania madarakani lazima uwe mkali.

Ban ametoa wito wa hatua za kuondolewa vizuizi vyote vilivyowekwa kwenye hotel ya Golf na vikwazo dhidi ya vikosi vya Umoja wa Mataifa nchini humo UNOCI,bwana Ouattara na wasaidizi wake wanakaa kwenye hotel ya Golf na kulindwa na wanajeshi wa UNOCI.