Skip to main content

Visa vingine 53 vya ubakaji vyafanyika DR Congo:UM

Visa vingine 53 vya ubakaji vyafanyika DR Congo:UM

Maafisa wa Umoja wa Mataifa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo leo wameripoti madai mengine 53 ya visa vya ubakaji Mashariki mwa nchi hiyo na kufikisha visa 120 tangu kuanza kwa mwaka huu.

Washutumiwa ni pande zote wakiwemo wanajeshi wa jeshi la serikali ya Congo. Kwa mujibu wa msemaji wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Congo MONUS wanatiwa hofu na ongezeko la vitendo vya ubakaji katika Kivu ya Kusini nay a Kaskazini, ubakaji unaodaiwa kufanywa na makundi yenye silaha ya kigeni nay a Congo pamoja na wanajeshi wa jeshi la serikali.

Visa ambavyo vimekwisha ripotiwa ni pamoja na vilivyofanyika siku ya mwaka mpya kwenye miji ya Fizi na Bushani ambako jeshi la serikali liitwalo FARD limeshutumiwa kuhusika na ubakaji wa watu 67, wanajeshi 11 wanashikiliwa kwa tuhuma hizo.

Lakini tangu wakati huo visa vingine 53 vya ubakaji vimefanyika katika eneo la Moyens Plateau ambavyo MUNUSCO inasema vinaaminiwa kufanywa na kundi la wapiganaji wa Kihutu kutoka Rwanda la FDLR.