Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM kutafiti athari za fedha zinazotumwa nyumbani Pakistan

IOM kutafiti athari za fedha zinazotumwa nyumbani Pakistan

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limezindua utafiti wa kutaka kubaini athari za fedha zinazotumwa nyumbani na wafanyikazi wahamiaji raia wa Pakistan wanaofanya kazi nchini Saudi Arabia kwa familia zao nyumbani.

Utafiti huo utasaidia washikadau serikalini kubuni sheria mpya za kuhakikisha kuwa fedha zinazotumwa nyumbani zimechangia maendeleo mashinani na hata kwenye ngazi za kitaifa. Kulingana na utafiti wa awali uliofanywa na IOM ulibainisha kwamba hali ya uchumi iliyoikumba dunia mwaka 2008 na 2009 ilikuwa na athari ndogo kwa kiwango cha fedha kinachotumwa kwenda nchini Pakistan.

Utafiti huo pia unapendekeza kuwa sekta ya benki nchini Pakistan inaihitaji kuimarika ili kuwavutia wahamiji kuitumia kutuma fedha nyumbani suala ambalo litasaidia fedha hizo kuchangia katika maendeleo ya Pakistan.